×

Anti Lulu aloweshwa, nguo za ndani zaonekana

IMG-20160329-WA0001
Msanii wa filamu ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ akilishwa keki kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Na Hamida Hassan
Msanii wa filamu ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kumwagiwa pombe na maji hadi kumfanya nguo zake za ndani zionekane.

Hayo yalimkuta mwanadada huyo kwenye pati yake za kuzaliwa iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Triple Seven, Mikocheni jijini Dar baada ya mashosti zake kumfanyia sapraizi.

IMG-20160329-WA0002….Akiwa chapachapa baada ya kumwagiwa pombe na maji.

Baada ya kufika eneo la tukio, Lulu alionekana mwenye furaha na mashosti zake walipoanza kumwimbia kale ka wimbo ka ‘hapi basdei tu yuu’ wakaibuka watu na kumwagia vimiminika vilivyomfanya aloe hadi kumfanya akose amani.

Hata hivyo, kwa kuwa tukio la kumwagiwa maji lilikuwa sehemu ya sherehe, hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuserebuka.
Akizungumzia eventi hiyo, Anti Lulu alisema: “Hili la kumwagiwa maji siyo ishu so niko poa ila nafurahi kutimiza miaka kadhaa, nimekua na nimebadilika sana.”

Leave a Comment