×

Aaiii… Wewee…!-4

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Kuchangamka kwa Msoba sasa wakati mwenzake alitamani kupumzisha akili, kuliibua utofauti katika mawasiliano ya mahaba kwani, Sanura alionesha waziwazi kwamba alikuwa amechoka sana….

SASA TAMBAA NAYO MWENYEWE…
Awali, Sanura alisema kama kumpasha tu habari Msoba lakini alipomwona kama hana dalili ya kumpumzisha akalifanya ombi lake kuwa suala la kitaifa.

Kwani alianza kusema kwa sauti kama anayetangazia jamii iliyowazunguka kwamba, alikuwa anabebeshwa mzigo asioumudu…
“Mpenzi, si basi jamani,” alilalamika Sanura, lakini Msoba hakumjibu kitu.
Ilifika mahali, Sanura akawa hasemi, hatikisiki, afumbui kinywa na wala harushirushi mikono…
“Sanura,” aliita Msoba akijua mpenzi wake huyo amezimia. Sanura hakuitika zaidi ya kutulia kimya, lakini pia Msoba alisema moyoni ni lazima afikie lengo lake kwanza ndipo atafute ufumbuzi wa mwanamke huyo.
Aligugumia maneno akiwa katika spidi kali na kumaliza mchezo, akajiegeza pembeni na kuita…
“Snura…we Snura…”
“Bee…”
“Vipi?”
“Poa tu. mimi mwenzako nakwambia nimechoka we husikii!”
“Sasa si nilikuwa bado.”
“Loo! Kumbe ningekuacha ulale tu…hivi unapata wapi stamina wewe Msoba?”
“Ni asili yangu…”
“Loo! Wewe…haya bwana.”
Walikumbatiana na kulala hadi asubuhi. Lakini wakiwa hawajaamka, waliongea kidogo…
“Hivi mpenzi wa Snura, huyo jamaa yako mliyetengana anaitwa nani?”
“Jalia…wewe je, mke uliyemwacha anaitwa nani?”
“Anaitwa Sada.”

***
Kwa upande wao, Sada na Jalia siku hiyo walichati kwa meseji za simu. Ikafika mahali, Sada akamuuliza Jalia…
“Hivi baby, mke uliyeachana naye anaitwa nani?”
“Anaitwa Sanura…wewe je, jamaa anaitwa nani?”
“Anaitwa Msoba.”
Ikawa Sanura yuko na Msoba bila Jalia kujua kuwa, Sada aliye naye mumewe ndiyo Msoba na wao akina Msoba na Sanura vilevile hakuna aliyejua kuwa, mwenzake wake yupo na mmoja wa kati yao.

***
Siku moja, Sada na Jalia wakwenda kuosha macho kwenye maduka ya Mlimani City. Katika pitapita, Sada alimuona Msoba, akamjulisha…
“Baby…baby, unamwona yule jamaa amevaa suruali ya jinsi na t-shirt ya njano?”
“Yeah! Vipi kwani…unamjua?”
“Sasa yule ndiyo Msoba.”
“Ala! Ndiyo imebaki kuwa stori tena,” alisema Jalia.
Msoba alimwona Sada akiwa na Jalia, akajua ndipo alipoamua kujituliza sasa.
Walipotoka  nje, Jalia akamwona Sanura amekaa kwenye mgahawa…
“Sweet…sweet…unamwona yule mdada amekaa pale kwenye meza ya peke yake amevaa suruali ya kitambaa na blauzi nyeupe?”
“Eee, yule…”
“Sasa yule ndiyo Sanura…sijui anasubiri mchongo gani pale?”
Sanura naye alimwona Jalia akamtumia meseji Msoba ambaye alikuwa bado ndani…
“Baby nimemwona Jalia, yuko na mwanamke wake nadhani…”
“Huyo mwanaume kavaaje baby?” aliuliza Msoba…
“Kavaa pensi ya jinsi na t-shirt nyeupe kubwa…”
“Haa! Ndiyo alikuwa mume wako huyo?”
“Yes d…”
“Sasa huyo mwanamke ndiye Sada aliyekuwa na mimi. Nimewaona huku ndani,” alisema Msoba, wote wakabaki kushangaa.
“Kwa hiyo Msoba na Sanura wakawa wamejua kuwa, Jalia ndiyo yuko na Sada kwa sasa lakini Jalia na Sada wao hawakujua kitu zaidi ya Sada kumwona Msoba ndani na Jalia kumwona Sanura nje.
Jalia na Sada nao wakaenda kukaa kwenye meza nyingine lakini bila kumsalimia Sanura ambaye naye hakutaka kusalimiwa na Jalia, walijengeana chuki kubwa wakati wa kuachana.

Baada ya muda, Msoba alitoka na kukaa na Sanura jambo ambalo sasa liliwashangaza Sada na Jalia…
“Khaa! Baby ina maana Msoba ndiyo yuko na mtalaka wako, naona amekwenda kukaa palepale lakini usigeuke kuwaangalia wasije wakasema tunawadiskasi wao,” alisema Sada akiwa anakunywa juisi.
“He! Makubwa hayo,” alishangaa Jalia…
Msoba yeye baada ya kukaa tu na kumwona Sada amekaa jirani pale, alisimama kuwafuata huku akitembea kwa mwendo wenye kisasi ndani yake.
Sanura alishangaa, akabaki ametoa macho kumwangalia atafanya nini…

Je, nini kiliendelea? Usikose kusoma wiki ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave a Comment