×

Tiwa Savage aibuka stejini na mwanaye

Tiwa_Savage's_studio_portraitMwanamuziki maarufu wa kike wa Nigeria, Tiwa Savage.

MWANAMUZIKI maarufu wa kike wa Nigeria, Tiwa Savage, hivi majuzi aliwashangaza mashabiki wake alipoibuka stejini kutumbuiza akiwa na mwanaye wa kiume aitywaye Jamil, ambaye alikuwa kivutio kikubwa alipofanya shoo ya nguvu.

Kituo hicho hicho ni mwendelezo wa wasanii kuibuka stejini na watoto wao, ambapo mwaka 2012, mwanamuziki Lauryn Hill wa Marekani, ambaye amewahi kutoa moja ya albam zenye kupendwa zaidi duniani, alipoibuka na watoto wake stejini.

Pulse-Tee-Billz-Tiwa-Savage-JamilTiwa akiwa na mwananye.

Tiwa ambaye alitamba stejini na mwanaye huyo, alimfanya shabiki mmoja kuandika kwenye mtandao: “Safi sana…… Lakini, anti Tiwa, kwa nini ulimficha sana mwanao uso wake kwa muda mrefu wakati ulijua kabisa mwishoni utamwonyesha? Karibu Naija (Nigeria), hata hivyo, hatuwalipi mastaa kutokana na sura za watoto wao. Ni picha nzuri”.

Leave a Comment