Magaga ni ugonjwa unaosababisha miguu kupasuka na wakati mwingine kufikia hatua ya kutoa damu. Leo ninawaletea tiba inayoweza kutibu tatizo hilo kwa kutumia chakula.
UNGA WA MCHELE
Wengi wameuzoea unga wa mchele kwa kupikia vitumbua, wengine hutumia kwa kuchanganya na unga wa mahindi ili kupika ugali na baadhi hupikia mikate.
Hayo ni matumizi ya kula, lakini kwa upande wa tiba husaidia kuondoa mpasuko wote wa gaga.
MAHITAJI
Kijiko kimoja cha asali, unga kiasi wa mchele, siki ya tufaha kijiko kimoja kidogo.
Ukimaliza changanya vyote kwa pamoja ili kupata mchanganyiko mmoja, kama miguu yako itakuwa imepasuka sana mpaka imefikia kutoa vidonda, changanya mchanganyiko huo na mafuta ya mrozi au ya mzaituni.
Baada ya hapo paka mchanganyiko wako kwenye mpasuko, kisha acha kwa muda wa dakika kumi, kisha chukua unga wa mchele uliolowekwa kwenye maji kidogo, uwe mzito kisha upake tena kwenye nyayo zako. Ukikauka sugua kama unafanya masaji, fanya hivi kila siku mpaka utakapoona tatizo limeisha.