
DORIS Mollel Foundation kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya simu ya Vodacom, jana waliazimisha siku ya Mtoto Njiti duniani maandimisho yaliyofanyika Jengo la Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), Profesa Barnabas Pembe aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Wageni wengine waalikwa ni pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Sister Zuhura ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengineo.
Katika maadhimisho hayo wataalamu mbalimbali walielezea changamoto za watoto njiti na jinsi ya kuzikabili.

Miongoni mwa wataalamu aliyeelezea jinsi ya kupunguza changamoto hizo ni Dkt. Augustine Massawe ambaye ni mshauri kitabibu wa Watoto Njiti ambaye amekuwa akiitwa jina la utani la Babu Njiti kutokana na kazi yake ya kuwahudumia watoto hao.
Babu Njiti alisema watoto hao ambao wanazaliwa kabla ya miezi tisa hivyo wanakuwa na changamoto nyingi kutokana na mfumo wa miili yao kutokamilika.

Baada ya hao kuzungumza mwazilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel aliwashukuru wageni wote pamoja na wataalamu walichangia katika kuelezea jinsi tutauavyoiweza kupambana na changamoto za watoto hao.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Doris alisema hata yeye alizaliwa njiti lakini amefanikiwa kukua salama mpaka kufikia hapo halipo ingawa si hilo tu lililomsababisha huruma ya kuanzisha taasisi ya kusaidia ukuaji wa watoto hao.

Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Kitengo cha Kusaidia Jamii, Sandra Oswald amesema kampuni yao imeamua kuungana na Doris Mollel Foundation kupitia kitengo chao cha kusaidia jamii ili kuokoa maisha ya Watoto ambao asilimia kubwa hufariki baada ya kuzaliwa kutokana na changamoto mbalimbali kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati.


Sandra amesema katika kitengo chao cha kusaidia jamii wamewekeza zaidi ya milioni 100 ili kusaidia mambo mbalimbali ikiwemo mpango za uzazi salama, Kudhibiti Fistula ambapo mpango huo umeshawasaidia kinamama zaidi ya 8000 nchini nchi nzima. Amesema Sandra. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA IMELDA MTEMA GPL