×

Droo ya 3 Shinda Nyumba

Makala: Andrew Carlos
WASHINDI waliopatikana katika droo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, iliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Manzese-Bhakresa jijini Dar, wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao Jumatano ya keshokutwa ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge.

Katika droo hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya watu, zawadi kwa mshindi wa kwanza ilienda kwa Zalika Ally (39) kutoka Lushoto, Tanga aliyejipatia runinga ya kisasa pamoja na King’amuzi cha Ting.

Akizungumza na Uwazi, Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema miongoni mwa watakaochukuwa zawadi zao kesho ni pamoja na wale walioshinda Ving’amuzi vya Ting, mashuka na simu ya kisasa.

“Bahati Nasibu hii ya Shinda Nyumba imezidi kuwaamsha watu wa mikoani na hii inathibitisha kwa washindi wanaoendelea kupatikana kila droo hizi zinapochezwa. Safari hii mshindi wa mashuka ametokea Handeni, Tanga ambaye ni Mkiwa R. Sendaro, vyombo vya jikoni vimeenda kwa Asha Musa Athuman wa Ruvuma huku mshindi wa kwanza Zalika Ally wa Lushoto, Tanga aliyejishindia runinga ya kisasa pamoja na King’amuzi cha Ting.

“Bahati Nasibu hii bado inaendelea na unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti pendwa yanayochapishwa na Global Publishers kisha jaza kuponi na kutuma,” alisema Mkanda.

Washindi wengine wanaotarajiwa kupokea zawadi zao kesho ni Isack Wilyady (Mikocheni, Dar), Majaliwa Temboko (Dar), Magreth Resiell Chacha (Pwani), David E. Kongola (Dodoma) na Pendo L. Mkonda (Iringa) waliojishindia Ving’amuzi vya Ting pamoja na Charles Elia Chawala kutoka Mbagala, Dar aliyejishindia simu ya kisasa.

Droo nyingine ya nne inatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu na droo ya mwisho itafanyika Juni ambapo mshindi wa zawadi kubwa atazawadiwa nyumba ya kisasa iliyopo Salasala-Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa na samani zake.

Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18 pamoja na ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki

Leave a Comment