×

Shinda Nyumba… Washindi Kukabidhiwa Zawadi Zao Leo

Na Andrew Carlos
WASHINDI wa droo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, wanatarajia kukabidhiwa zawadi zao leo katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar.

Droo ya tatu ya bahati nasibu hiyo iliendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese jijini Dar ambapo Zalika Ally kutoka Tanga alijishindia zawadi kubwa ya TV Flat Screen pamoja na King’amuzi cha Ting huku washindi wengine wakijizolea zawadi kibao kama seti ya vyombo vya jikoni, simu za kisasa za mkononi (smart phone) pamoja na mashuka.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema kuwa bado kila mmoja ana shauku ya kushiriki na kushinda hivyo ofisi bado inaendelea kupokea kuponi nyingi kutoka kwa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa na Risasi.

“Zoezi zima la utoaji wa zawadi kwa washindi waliopatikana wiki iliyopita linatarajiwa kufanyika leo na niwaombe wasomaji wengine wote, bado shindano hili linaendelea na droo zake kabla ya kufikia droo kubwa itakayofanyika Juni, mwaka huu hivyo endelea kununua magazeti ya Global na kukata kuponi ndani yake,” alisema Mkanda.

Washindi wengine wanaotarajia kuchukua zawadi zao leo ni pamoja na Mkiwa R. Sendaro wa Handeni, Tanga aliyeibuka na mashuka, Charles Elia Chawala aliyejishindia simu ya kisasa, Isack Wilyady (Mikocheni, Dar), Majaliwa Temboko (Dar), Magreth Resiell Chacha (Pwani), David E. Kongola (Dodoma) na Pendo L. Mkonda (Iringa) waliojishindia Ving’amuzi vya Ting.

Droo kubwa inatarajiwa kufanyika Juni mwaka huu ambapo mshindi wa zawadi kubwa atajinyakulia nyumba ya kisasa yenye samani zake iliyopo Salasala-Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18 pamoja na ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki.

Leave a Comment