×

Magufuli atengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga

12961631_885964771514498_7904324691807387157_n

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr.John Pombe Magufuli alipomuapisha Ana kilango Malecela kuwa Mkuu wa mkoa wa shinyanga.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ana kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave a Comment