×

Wabunge wa jumuiya ya africa mashariki kuhamasisha fursa za kibiashara

1.Mbunge wa Bunge la Arika Mashariki, Addullah Mwinyi (katikati) akizungumza jambo katika mkutano huo na wanahabari.Hawapo pichani.-001Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi (katikati) akizungumza jambo katika mkutano huo na wanahabari (Hawapo pichani).

2.Kutoka kushoto ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Makongoro Nyerere na Abdullah Mwinyi wote wakiwa ni wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.-001Kutoka kushoto ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Makongoro Nyerere na Abdullah Mwinyi wote wakiwa ni Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

3.Baadhi ya wanahabari wakichukua tukio hilo.-001Baadhi ya wanahabari wakichukua tukio hilo.

WABUNGE wa Jumuiya la Afrika Mashariki wamesema wataanza kuhamasisha jamii ili kujua fursa za kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa leo hii jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo  amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika Soko la Kariakoo na Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na kutumia vyombo vya habari katika kufikisha taarifa kwa umma.
Mwinyi  amesema kusudi lao ni kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Alifafanua kuwa fursa mbalimbali zipo kwa walimu wa wanaofundisha Kiswahili ambapo wanaweza kwenda kufundisha lugha hiyo kwenye Nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya Kati.

Aliongeza kuwa Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndiyo fursa kubwa tuliyonayo hapa nchini ambayo inaweza kuwasaidia wataalamu wa lugha hiyo kupata ajira.

NA DENIS MTIMA /GPL

Leave a Comment