Stori: Andrew Carlos, UWAZI
MSHINDI wa king’amuzi cha Ting katika Droo ya Tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers, Isaac Williard Kapili ametoboa siri ya ushindi iliyompatia zawadi hiyo kuwa hadithi ndizo zilizomfanya kununua magazeti mengi na ilipokuja bahati nasibu hiyo ikampa hamasa zaidi ya kuyasoma.
Katika droo hiyo iliyofanyika hivi karibuni na washindi kukabidhiwa zawadi zao ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar, Isaac alisema kuwa ameshiriki mara nyingi na safari hii Mungu amemuita kwani ulikuwa ni wakati wake kushinda.
“Hakuna mbili bila kuwa na moja, nimeanza na moja na mbili itakuwa kwangu tena. Ujue hakuna kitu kinachokupa furaha kama kupata bahati, kitendo cha kupata bahati ya kuwa mshindi tu ni furaha tosha kwangu,” alisema Isaac.
Katika droo hiyo, mshindi wa zawadi kubwa ambayo ilikuwa TV Flat Screen alikuwa ni Zalika Ally wa Lushoto mkoani Tanga huku zawadi nyingine kibao zikitolewa kwa washindi kama vile ving’amuzi vya Ting, dinner set, bed sheet, smartphone na nyingine nyingi.
Droo kubwa inatarajiwa kufanyika Juni mwaka huu na zawadi kubwa itakuwa ni nyumba ya kisasa yenye samani ndani iliyopo Salasala, Kinondoni jijini Dar.
Wafanyakazi na ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers na wote walio na umri chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.