×

Mbunge adaiwa kuzaa na bintiye

stori:  Mwandishi wetu, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Aibu kubwa! Habari zilizotua kwenye dawati la Ijumaa hivi karibuni zinasema kuwa, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalo) kutoka mkoa mmoja wa kanda ya kati, anadaiwa kuzaa na binti yake, twende na Ijumaa.

Kwa mujibu wa chanzo, uhusiano wa kimapenzi kati ya mbunge huyo na binti yake aliye katika masomo kwenye chuo kimoja kilichopo Dodoma, ulianza wakati mama mtu alipokwenda nchini India kwa matibabu.
“Hivi mnaijua ishu ya mbunge…(anamtaja jina) kuzaa na binti yake aitwaye…(jina)? Kama hamna habari basi mimi nawapeni.

“Mwaka 2014, mke wa huyu mheshimiwa alipata tatizo kwenye mguu wake wa kulia, ikabidi aende India. Safari ya India aliongozana na dada yake, yaani shemeji wa mbunge.

“Huku nyumbani, mzee akabaki na bintiye ambaye alikuwa likizo ya chuo. Ghafla majirani wakaanza kuhisi kwamba mbunge anatembea na mwanaye kwani mara nyingi jioni walikuwa wakitoka wote na kurudi usiku mwingi huku wamelewa.
“Baadaye ikawa siyo siri tena! Msichana wao wa kazi akawa anawashangaa wanavyoitana dear wakati ni baba na binti yake,” kilidai chanzo hicho.

Kiliendelea kudai kuwa, mama mtu aliporejea kutoka India, binti huyo alikuwa amesharudi chuoni lakini baada ya miezi minne alirudi nyumbani akiwa mjamzito.

“Sasa kazi ikawa ni mimba ya nani! Binti alimlinda baba yake kwa kumtaja mfanyabiashara mmoja wa mjini Dodoma aitwaye Cosmas. Kwa hiyo mpaka alipojifungua, mama anajua mwenye mtoto ni Cosmas ingawa hajawahi kumwona hata siku moja.

“Watu mtaani wanajua mtoto ni wa mbunge lakini mke hajui kitu na hakuna wa kumwambia. Yule msichana wa kazi alitimuliwa kipindi kilekile mke yuko India. Ila baba anampenda sana binti yake, kila anachotaka anapewa, nadhani kwa sababu ya kumfichia siri.

“Hivi karibuni nimesikia binti anataka kurudi tena chuo maana mtoto amekomaa. Ana miaka miwili hivi. Hebu fuatilieni wenyewe kwa kina mtuletee uhondo,”  kilisema chanzo hicho.

Juzi, Ijumaa lilimsaka mbunge huyo kwa njia ya simu lakini muda mwingi iliashiria inaongea. Gazeti linaahidi kuendelea kuifuatilia habari hiyo.

Leave a Comment