×

Shika Ndinga na Efm yatikisa Ilala

1Mmoja ya washiriki aliyeibuka kuingia katika mzunguko wa tano, akishiriki shindano hilo.

2 Mshiriki, Saidi Abdalah akichuana vikali kwenye mzunguko wa mwisho wa Shika Ndinga.

3 Washindi wa shindano hilo walioibuka kidedea jana, Said Abdallah (kushoto) na Zainabu Mhaghama wakiwa katika pikipiki zao.

4 Msanii wa kisingeli, Man Fongo, akitoa burudani kwenye shindano hilo.

5Mmoja wa wasanii  akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

6Mshiriki akiwa katika mapumziko.

7Baadhi ya wafanyakazi wa Efm Radio wakiwa katika pozi.

8  Watoa huduma ya kwanza wa Msalaba Mwekundu wakiwa viwanjani hapo ili kusaidia  atakayepatwa na tatizo.

9  Baadhi ya washiriki wakijianda na mashindano.

10Mwakilishi kutoka Vodacom akikabidhi zawadi ya simu kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

11 Washereheshaji wa shindano hilo la  Shika Ndinga wakitoa burudani ya aina yake, Swebe Santana na Chogo.

SHINDANO la Shika Ndinga  linaloratibiwa na kituo cha Redio Cha Efm  kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam, jana limezidi kutikisa katika viwanja vya Shule ya Msingi Tabata, Dar.

Shindano hilo limeendelea ikiwa ni mara ya pili sasa baada ya kufanyika wiki iliyopita kwenye viwanja vya Mbagala-Zakhem na kupatikana washindi, ambapo kwa wiki hii limezikutanisha kata zote za Wilaya za Ilala, Dar na kupatikana washindi wawili, Said Abdallah na Zainabu Mhaghama.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Efm Radio, Dennis Ssebo, alisema kuwa shindano hilo litaendelea  na washiriki 60 kwenye kila wilaya ambapo washiriki 10 kati yao  wanawake watano na wanaume watano wataingia katika fainali kujinyakulia gari aina ya Suzuki Carry.

Akikabidhi zawadi kwa washindi waliopatikana jana katika shindano hilo Ssebo alisema kuwa wiki ijayo litafanyika Wilaya ya Kinondoni kwenye Viwanja vya Biafra, huku akisisitiza wakazi wa wilaya hiyo kuendelea kusikiliza vipindi vya Efm Radio.

Kwa upande mwingine alisema lengo la shindano hilo ni kuwawezesha wasikilizaji wa Efm  kwa namna moja au nyingine kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.

Picha na: Hilaly Daud/Gpl

1 Comment

Leave a Comment