×

‘Maajabu’ daraja la Kigamboni


KG1

Daraja la Kigamboni.

Sifael paul, Risasi mchanganyiko

Dar es Salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ jana alitarajiwa kuzindua rasmi Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi ambapo Risasi Mchanganyiko linakujuza maajabu yake.

Kabla ya uzinduzi huo, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakazi wa Dar walipata fursa ya kulitumia daraja hilo na kujionea urahisi uliopo kwa sasa wa kuvuka kwenda na kurudi Kigamboni bila tozo za magari huku maguta na mikokoteni vikiwa haviruhusiwi.

JK+Nyumba+NHC+Photo

Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Magari yaliyoruhusiwa kupita kwenye daraja hilo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10 ili kusaidia upitaji wa magari katika barabara ya juu (interchange) kwenye eneo la Kurasini.

Kuhusu madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia sheria ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu wa miundombinu ya daraja hilo.

Wasimamizi wa daraja hilo wanasimamia madereva kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi huku kila kitu kikionekana kwenye kamera za kumwaga zilizofungwa darajani hapo.

Leave a Comment