×

D’banj: Sikumuondoa Tonto Dikeh Kwenye Lebo Yangu

Dbanj-Tonto-Dikeh

D’banj na Tonto Dikeh

LAGOS, Nigeria

BOSI wa Lebo ya DB Records, D’banj, ameibuka na kusema wala hakumuondoa msanii ambaye pia ni muigizaji kutoka Nollywood, Tonto Dikeh kwenye lebo yake na kwamba ni yeyé mwenyewe ndiye aliamua kuondoka lakini anaamini kuwa atarejea.

Tonto Dikeh, 30, alitangaza kuondoka kwenye lebo hiyo baada ya kufunga ndoa na mumewe, Oladunni Churchill ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aliyekuja duniani Februari mwaka huu.

Akizungumza na mtandao mmoja wa kiburudani wa Nigeria, D’banj alisema hajawahi kumuona Tonto Dikeh tangu alivyoolewa lakini anadai mara ya mwisho alimwambia kuwa anataka kufanyakazi kwenye taasisi yake.

“Sijamuona tangu alivyoolewa na sasa ukiangalia ana mtoto. Aliondoka hapa nchini na mara ya mwisho aliniambia anataka kufanya kazi kwenye taasisi yake. Ninaamini kama atarudi basi tutafanya maamuzi,” alisema D’banj.

Tonto Dikeh ngoma yake ya kwanza aliitoa Oktoba mwaka 2012, aliyoipa jina la Hi and Itz Ova, kabla ya mwaka 2014 kusaini kwenye Lebo ya DB.

Leave a Comment