Kwa mwanamke kuolewa ni heshima kubwa! Ndiyo maana leo hii wapo wanaohangaika kwa waganga na kufanya kila linalowezekana ili nao waingie katika ile orodha ya wake za watu.
Kuolewa sasa hivi imekuwa dili sana hasa kwa mastaa. Ikitokea staa akapata bahati ya kumpata mwanaume, akamvisha pete kisha akaolewa inakuwa ni furaha ya aina yake hasa kutokana na ile dhana kwamba mastaa hawaoleki.
Lakini wakat
kukiwa na dhana hiyo, wapo ambao wanabahatika kupata wanaume wa kuwaoa lakini kudumu kwenye ndoa inakuwa ni mtihani wanaofeli. Mifano ya mastaa wa kike walioingia kwenye ndoa kisha kutoka iko mingi sana.
Hata hivyo, tunapozungumzia mastaa waliowahi kuolewa kisha wakaachika, Wastara Juma na Khadija Shaibu ‘Dida’ wanaweza kuwa wameweka rekodi ya Bongo kutokana na idadi ya ndoa walizonazo hadi sasa.
Wazungu wana msemo wao usemao ‘Too much is harmful’ wakimaanisha kwamba, kila kitu kikizidi kipimo haifai. Kuolewa na kuachika wala siyo jambo la ajabu kwani wanawake wengi wamepitia huko kutokana na sababu mbalimbali.
Kwamba unaweza kuwa umeingia kwenye maisha ya ndoa na mwanaume ambaye ni pasua kichwa, ukashindwana naye na ukaamua kutoka kwenye ndoa.
Ila sasa ile leo umeol
kesho umeachika, keshokutwa umeolewa, mtondogoo umeachika, hapo ndipo penye tatizo. Hilo ndilo linalowaganda Dida na Wastara kwamba ile kuolewa na kuachika kwao imekuwa ni ‘too much’, hadi
wenye matatizo na siyo wanaume wanaowaacha.
Tuanze na Dida
Katika historia ya maisha yake inaonekana aliwahi kuolewa na wanaume watatu. Wa kwanza ni aliyefahamika kwa jina la Mohammed Mchopanga ‘Mchops’ ambaye Dida alimpaisha sana kwa kujiita Dida wa Mchops.
Mume wa pili wa Dida ni Gervas Mbwiga ‘G’. Mbwembwe za kumtangaza mwanaume huyo zikaanza, akajibadili jina na kujiita
Dida wa G. Hata hivyo, wakaachana mwaka 2014 kabla ya Mtangazaji Ezden Jumanne kuchukua kijiti kabla ya kumwagana mwaka 2015.
Hivi karibuni zimevuja taarifa kuwa amepata mwanaume mwingine aitwaye Issa Selemani na wanatarajia kufunga ndoa.
Wastara naye
Huyu aliwahi kufunga ndoa ya kwanza mwaka 1998 na mwanaume aitwaye Juma Mpemba. Ndoa hiyo haikudumu kwani aliachika kabla ya mwaka 2000 kuolewa tena na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ahmed Kushi.
Kwenye rekodi haionekani walidumu kwa muda gani ila ilipofika mwaka 2009 alifunga ndoa na marehemu Sadick Juma ‘Sajuki’. Ndoa hiyo ilitenganishwa na kifo cha Sajuki ambapo kwa Wastara alisema asingempata wa kuziba pengo la mumewe huyo.
Hata hivyo, hivi karibuni alipata bahati tena ya kuolewa na mwanasiasa Juma Sadifa, ndoa iliyodumu kwa miezi miwili tu kabla ya kupinduka chali.
Kwa rekodi hizo utaona ni kwa jinsi gani wanawake hao wamekuwa wakipata bahati ya kuolewa lakini kuzishika ndoa zao limekuwa jambo gumu na leo hii wanaonekana ni mastaa wanaongoza kwa kuingia kwenye ndoa na kutoka.
Mastaa wengine waliowahi kuolewa na kuachika ni pamoja na Lady Jaydee, Davina, Nora, Aunt Ezekiel na Skaina hata hivyo na wao huenda ndoa ziko njiani kwani ni jambo la heri na lililoamrishwa na Mwenyezi Mungu