×

Juisi ya bizari ya manjano kwa kukata tumbo

binzari

Wiki hii kwenye ukurasa wetu huu wa urembo nitakupa njia ya kuondoa mafuta tumboni pamoja na kukata tumbo kwa kutumia juisi ya bizari ya manjano.

Mahitaji
Nusu kijiko kidogo cha bizari manjano
Tangawizi
Ndimu kipande
Maji nusu glasi
Ndizi moja

Jinsi ya kuiandaa
Chukua ndizi, ioshe kisha isage kwenye maji safi uliyoandaa, chukua tangawizi ya unga kidogo uchanganye na ndimu kipande kimoja kisha weka kijiko kidogo nusu cha bizari ya manjano utapata juisi nzuri.
Kunywa juisi hii baada ya kula chakula ni nzuri kunywa muda wa kulala ili ifanye kazi haraka.
Jinsi inavyofanya kazi
Juisi hii inasaidia kusafisha ini, inakata mafuta na kusaidia kusaga chakula haraka.

Leave a Comment