Mwanamuziki Tyrese Gibson hivi karibuni alisilimu na kuwa Muislamu na mara kadhaa amekuwa akieleza jinsi alivyokuwa akimuomba Mungu aingie kwenye hatua hiyo.
Kuonesha kuwa anataka ulimwengu ujue kuwa ameingia kwenye dini hiyo akiwa tayari kufuata taratibu zote, juzikati alitupia picha akiwa anaswali msikitini.
Picha hiyo inamuonesha akiwa anasujudu kisha akasindikiza na maneno yaliyosomeka: ‘Siku ya kwanza kuingia msikitini mapigo ya moyo yalikuwa yakienda mbio. Nilifundishwa jinsi ya kuswali na nikajihisi niliyebarikiwa. Mwenyezi Mungu abariki mawazo yangu.’