Na Hamida Hassan
Msanii wa Filamu za Bongo, Vanita Omary juzikati alijikuta akipagawishwa na keki sita ambazo alizawadiwa na marafiki zake kwenye siku yake ya kuzaliwa hali iliyomfanya abaki ameduwaa asijue akate ipi.
Katika sherehe hiyo iliyofanyika nyumbani kwake alipokuwa amealika watu wachache, Vanita alijikuta ameduwaa kwani kila aliyeleta alitaka yake ndiyo ikatwe lakini mwisho wa siku alikata moja na kuwalisha marafiki zake.
“Unajua kila aliyeleta keki alitarajia nikate yake, sasa zilivyokuwa nyingi vile nikashindwa nimfurahishe yupi, mwisho nikafanya uamuzi bila kujali,” alisema Vanita.
