×

Niyonzima: Simba mmetupa Kessy! Mmeumia

-6424Haruna Niyonzima

Said Ally,
Dar es Salaam
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ametamka kuwa wataendelea kuwafunga Simba na kuendelea kuwasumbua wapinzani wao hao kutokana na tabia yao ya kuwapa wachezaji wanaokuwa muhimu katika kikosi chao.

Niyonzima ameyasema hayo ikiwa ni baada ya siku chache Yanga kumalizana na aliyekuwa beki wa Simba, Hassan Kessy na kumpa mkataba wa miaka miwili huku akivuna milioni 40 za usajili wake.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema kuwa tabia ya viongozi wa Simba kuachana vibaya na nyota wao kama ilivyokuwa kwa Kessy, ndiyo ambayo imekuwa ikiwafanya wao Yanga waendelee kuwa imara zaidi na hatari zaidi ya wapinzani wao ambao wanaendelea kusota bila kutwaa ubingwa kwa msimu wa nne sasa.

“Nimekuwa najua jinsi Kessy anavyocheza kwa kipindi kirefu na kuja kujiunga kwetu hilo ni jambo zuri na ambalo naona kuwa litatufanya tuwe na makali zaidi katika msimu ujao, maana tunaendelea kuwa na nyota wakali na wenye vipaji vya hali ya juu.

“Kwa kupitia yeye naona kuwa tuna nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wetu na hiyo inasababishwa na hasira za viongozi wa Simba ambao wamekuwa wakitupa nguvu kwa kutupa wachezaji mahiri kama ilivyo kwa Tambwe (Amissi)na sasa Kessy,” alisema Niyonzima.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment