MWANAMUZIKI mkongwe, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ a.k.a Oil Chafu katika kukamilisha utambulisho wa kurejea kwake katika ‘game’, amepanga kufanya shoo kubwa wikiendi hii itakayokwenda kwa jina la Usiku wa Mamba.
Katika shoo hiyo itakayofanyika Jumapilli hii kwenye Ukumbi wa Maisha Basement, Dar es Salaam, Dudu atasindikizwa na Amini na wasanii wengine watakaokuwa ‘surprize’ kwa mashabiki watakaojitokeza katika usiku huo.
“Itakuwa shoo babkubwa yenye kiingilio cha Sh 10,000 na yatakayofanyika humo yatamkuna kila mmoja, kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kupigwa jukwaani kwa ngoma ya Kokoriko pamoja na shoo nyingine za wasanii wakali zitakazokuwa surprize kwa mashabiki wote,” alisema Dudu.
