Stori: Hamida Hassan, Wikienda
Dar es Salaam: Mtangazaji wa Redio Choice FM ambaye ni msanii Bongo Fleva aliyeiwakilisha Tanzania kwenye Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013 ‘The Chase’, Feza Kessy, amefunguka kuwa anahisi mavazi yake yanayomfanya kuwa na muonekano wa kiume ‘Ki-Tommy Boy’ umemfanya aogopwe na wanaume kwani ameshatoka kimapenzi mara tatu na kuachana na wanaume aliokuwa nao.
Feza alisema uvaaji wake huo aliuanza tangu utotoni na anahisi ndiyo sababu ya yeye kushindwa kudumu kwenye uhusiano kwani mwanaume huhisi siku moja atadundwa.
“Kuna mmoja aliwahi kuniambia kuwa yeye ameshindwa kuwa na uhusiano na mimi kutokana na hali hiyo, hivyo tuliachana na alioa mwanamke mwingine,” alisema Feza ambaye uchumba wake na mshiriki mwenzake wa BBA, Oneal wa Botswana ulivunjika.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz