×

Vodacom, Global wawasogeza wasanii kwa mashabiki wao

 MSANII WAKO LAUNCH (16)

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya Staa Wako leo katika Makao Makuu ya kampuni hiyo eneo la Mlimani City jijini Dar. Kulia ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho na kushoto ni msanii Kajala Masanja.

MSANII WAKO LAUNCH (6)

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Global ilivyojipanga kuendesha huduma hii kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania.

MSANII WAKO LAUNCH (10)

Msanii Kajala Masanja (katikati) akielezea umuhimu wa huduma ya Msanii Wako iliyozinduliwa leo. Kulia ni Matina Nkurlu na msanii Aunty Ezekiel (kushoto).

MSANII WAKO LAUNCH (11)

Msanii Shilole ‘Shishi Baby’ akiwataka mashabiki wake kujiunga na huduma ya Staa Wako kwa kutuma neno SHILOLE kwenda 15542 ili wapate habari zinazomhusu.

MSANII WAKO LAUNCH (12)MSANII WAKO LAUNCH (1)

Wanahabari wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu .

MSANII WAKO LAUNCH (17)

Matina Nkurlu akiagana na Kajala Masanja (katikati) baada ya uzinduzi huo. Wengine pichani kutoka kulia ni Abdallah Mrisho, Shilole na Aunty Ezekiel.

 MSANII WAKO LAUNCH (5)

Matina Nkurlu akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Pembeni ni Abdallah Mrisho.

  MSANII WAKO LAUNCH (13)

Abdallah Mrisho akitoa ufafanuzi kwa wanahabari jinsi mashabiki wanavyoweza kujiunga na Staa wao.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Global Publishers & General Enterprises Ltd, leo wamezindua huduma itakayowawezesha wateja wake kupata habari juu ya maisha ya kila siku ya wasaniii mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya Vodacom yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, alisema huduma hiyo itagharimu kiasi cha shilingi mia moja tu (100/=) kwa siku, ambapo mteja atakuwa akipokea taarifa za msanii aliyemchagua kila siku kwa bei hiyo.

“Ili kujiunga na huduma hii, mteja anatakiwa kutuma jina la msanii mfano, Shilole au Kajala kwenda namba 15542, na hapo moja kwa moja atakuwa amejiunga na kuanza kupata habari za msanii husika.

“Kila siku mteja atakuwa anakatwa Sh 100 kwa ajili ya huduma hiyo, pia kwa kiwango hicho cha fedha kwa siku moja anaweza kupata taarifa za msanii huyo kadiri zitakavyokuwa,” alisema Nkurlu.

Aidha, alifafanua kuwa huduma hiyo inalenga kuwaunganisha wateja wa Vodacom na wasanii wao pendwa ili kuwaweka karibu, hiyo ikiwa ni jitihada zao kabambe za kutumia teknolojia kurahisisha na kufanya maisha kuwa murua.

Aliongeza kuwa japokuwa huduma hiyo imeunganishwa moja kwa moja, lakini mteja bado anao uwezo wa kujiondoa wakati wowote.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho, alisema hatua hiyo ni nzuri kwani kutokana na jinsi teknolojia inavyokua, hawana budi kuwakutanisha wasanii na mashabiki wao kwa njia yoyote ile lengo likiwa ni kuongeza ukaribu wao.

Katika hatua nyingine, Mrisho aliwataja baadhi ya wasanii ambao tayari wameshaingia kwenye mfumo huo kuwa ni Kajala Masanja, Wema Sepetu, Aunty Ezekiel, Jacqueline Wolper, Shilole na Rose Ndauka na kuongeza kuwa wapo kwenye mazungumzo na wasanii wengine na wana imani wasanii hao wataongezeka.

NA DENIS MTIMA/GPL

JINSI YA KUJIUNGA NA STAA WAKO;

WEMA SEPETU

Tuma neno WEMA kwenda 15542

ROSE NDAUKA

Tuma neno NDAUKA kwenda 15542

AUNTY EZEKIEL

Tuma neno EZEKIEL kwenda 15542

SHILOLE

Tuma neno SHILOLE kwenda 15542

KAJALA MASANJA

Tuma neno KAJALA kwenda 15542

JACQUELINE WOLPER

Tuma neno WOLPER kwenda 15542

Leave a Comment