MKALI wa vichekesho vya jukwaani, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kwa mara ya kwanza kesho (Juni 3) anatarajiwa kuibukia Mbeya na kuwavunja mbavu wakazi wa mkoa huo ndani ya Ukumbi wa Tugimbe Mafiati.
Akizungumza na mtandao huu, MC Pilipili ambaye ni mkali wa vichekesho vya jukwaani alisema, shoo yake hiyo itakwenda kwa jina la Cheka Vicheko vya Juu Nyanda za Juu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
“Baada ya kutikisa Mkoa wa Dodoma nimehamia kwa wakazi wa Mbeya ambapo nitawavunja mbavu mwanzo mwisho pale Tugimbe,” alisema MC Pilipili. Shoo hiyo itasindikizwa na mkali wa Bongo Fleva, Elius Barnaba.
