IMEBAINIKA! Kumbe msanii ambaye ni zao la Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond ameshiriki katika kuweka mistari yake katika Wimbo wa Zigo (remix) wa AY, My Life ya Dogo Janja pamoja na Make Me Sing wa Diamond.
Akizungumza katika Kipindi cha The Playlist kinachorushwa na Lil Ommy kupitia Times FM mwishoni mwa wiki iliyopita, Raymond anayetamba na Wimbo wa Natafuta Kiki alisema kuwa bosi wake (Diamond) ndiye alimpa nafasi ya kuweka mistari katika nyimbo hizo.
“Kuna baadhi ya melodi katika Wimbo wa Zigo (remix) kama ile ya mukidi mukide nilisaidia ambapo niliona kama ikikaa pale inakuwaje, wakaipokea,” alisema Raymond.
Raymond alisema pia ametoa mchango katika nyimbo kibao kama My Life ya Dogo Janja pamoja na Make Me Sing.