×

Mademu wa Kibongo wamdatisha Prezoo

prezzo (2)Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi

RAPA kutoka Kenya mwenye ‘kiki’ Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’ amedai kuwa ingawa yuko kwenye uhusiano wa mapenzi na mchumba wake Michelle Oyola aliyemvisha pete hivi karibuni lakini kutoka moyoni mwake anapagawishwa sana na mademu wa Kibongo.

Akichonga na Risasi Jumamosi, Prezzo ambaye yupo Bongo kwa ishu za kikazi ikiwa ni pamoja ya kukamilisha kolabo yake na Barakah Da Prince alisema kuwa ukiachana na Wema Sepetu aliyewahi kula naye ‘good time’ kwenye ulimwengu wa malavidave wapo mademu wengi nchini wanaomvutia jambo linalomfanya mara kwa mara kutembelea Bongo.

 “Unajua Tz imebarikiwa sana kiukweli, kuna mademu wazuri aisee,” alisema Prezzo.

Leave a Comment