Muhammad Ali enzi za uhai wake.
Bondia bingwa wa zamani wa dunia, Muhammad Ali ‘The Greatest’ amefariki dunia jana Ijumaa akiwa kwenye Hospitali ya Phoniex alipokuwa akitibiwa tatizo la mapafu. Muhammad amefariki akiwa na umri wa miaka 74.
Akiwa na watoto wake, Laila (kushoto) na Hana (kulia)
Muhammad alifikishwa kwenye Hospitali ya Phoniex iliyopo Jimbo la Arizona juzi Alhamisi baada ya kuzidiwa huku akiwa anapumua kwa shida na kikohozi kikali cha mara kwa mara. Mbali na tatizo la mapafu, Muhammad amekuwa akisumbuliwa na tatizo lingine kubwa zaidi kwenye mfumo wa fahamu ‘nervous system’ ambalo kitaalam linajulikana kama Parkinson.
Mbali na kunyakuwa mara tatu taji la Bondia Bingwa wa Ngumi za Uzito wa Uzani wa Juu wa Dunia ‘World Heavyweight Champion‘, Muhammad alikuwa ndiye bondia bora wa muda wote wa dunia.
Muhammad Ali alikuwa mtu wa kujigamba kupita kiasi, lakini alikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo. Alikuwa na kipaji cha pekee kwenye ndondi, alikuwa na kasi sana na nguvu pia. Alianza kujulikana aliposhinda dhahabu Michezo ya Olimpiki ya Roma 1960.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky na kuongeza kwamba alipozaliwa alipewa jina la Cassius Marcellus Clay.
Muhammad Ali alijiunga na masumbwi kwa bahati.
Ali aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikuwa na marafikize waktafuta peremende na porp corns za bure.
Na alipogundua kwamba baiskeli yake imeibwa aliagizwa kwende chini ya nyumba aliyokuwepo katika taasisi ya mafunzo ya Columbia ambapo afisa wa polisi Joe Martin alikuwa akisimamia mpango wa ndondi.
Martin alimwelezea Ali kwamba angeanza kunoa ngumi zake kwa kujifunza ndondi kabla ya kumtafuta mwizi huyo.
Kwa haraka alijua vile ambavyo angejichukulia na alipofika umri wa miaka 18 alikuwa ameshinda dhahabu ya Olimpiki mjini Rome.
…akiwa na mwanaye, Laila aliposhinda ubingwa wa ngumi uzito wa kati.
Alipata umaarufu mkubwa aliposhinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyiwa Roma mwaka 1960 katika uzani wa uzito wa kadri au light-heavyweight.
Alipewa jina la Utani “The Greatest” na alimtandika makonde Mmarekani mwenzake Sonny Liston mwaka wa 1964 na kushinda taji lake la kwanza la Dunia.
Alikuwa bondia wa kwanza kushinda taji la Heavyweight mara tatu.
Alistaafu mwaka 1981 baada ya kushinda mashindano 56 kati ya 61 aliyoshiriki.
Mohammed Ali alikuwa mkereketwa wa haki za kibinadamau ambapo atatambuliwa kukabiliana na ubaguzi wa rangi na ushairi wa kuvutia.
Alipoulizwa angalitaka kukumbukwa vipi alisema wakati mmoja: “Kama mtu ambaye hakuwahaini watu wake. Na ikiwa hilo haliwezekani basi nijulikane tu kama mwanandondi mzuri.
Sijali hata usipotaja nilivyokuwa mwenye umbo la kuvutia.”








INNA LILLAH WAINNA ILAHI RAJUUN…