×

Ili Uichukue Nyumba… Sikia Siri Hii Usiyoijua

NYUMBA (17) 

Na Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko

NAAMINI kila mmoja anaufahamu ule usemi maarufu wa bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi. Unajua kisa chake? Kuna visa vingi vinavyounga msemo huu na miongoni ni hivi;

Mtu mmoja alikuwa ametoka katika vikao vile vya jioni na aliporudi kwake alikuwa ameburudika kidogo, mwenyewe akisema ni kujisahaulisha na maisha magumu aliyokuwa akiishi, hohehahe.

NYUMBA (16)Kwa uchovu na mawazo, akajikuta amesinzia bila kufunga mlango wake. Usiku mnene, mwizi mmoja alivunja nyumba mtaa wa tatu, akafanikiwa kupata begi lenye fedha nyingi, lakini alipoanza kuondoka tu, wenyewe wakamkurupua, akaanza kutimua na begi lake mkononi.

Kona mbili tatu, begi likawa mzigo, lakini kuliko kuliachia kwa wenyewe, alipopita kwenye nyumba yenye mlango wazi, akalitupia lile begi mwenyewe akiendelea na mbio kukwepa kipigo na kifo.

SHINDA NYUMBA (3)Kishindo cha begi kikamshitua mwenye nyumba, akakurupuka na kupatwa na mshangao mkubwa kuona ametupiwa begi, lakini pia akasikia vishindo vya watu wakikimbia nje huku wakipiga kelele za mwizi, mwizi, mwizi.

Akanyata na kuufunga mlango wake, kisha akalifuata begi lile, akalifungua. La haula, mzigo mkubwa wa hela ulikuwa ndani yake, akapatwa na kiwewe kwa kuuaga umaskini kwa namna ya ajabu kabisa.

Ni kwa fedha hizo, maisha yake yakabadilika tangu siku hiyo na tunavyozungumza, alijiwekea msingi mzuri wa familia yake ambayo hadi sasa ina maisha mazuri.

Simulizi hii ina mafunzo mengi kwako wewe msomaji unayesoma hapa kwamba katika maisha, lolote linaweza kutokea endapo ukimtanguliza Mungu.

Fikiria, kwa kawaida mtu yule aliyeacha mlango wazi, alipaswa kuvamiwa, kupigwa na hata kuibiwa (ingawa alikuwa fukara), lakini Mungu akabadili kibao na kuufanya usahaulifu wake kumletea neema.

Hii inakufundisha kuwa mtu mwenye kuamini katika makusudi ya Mungu. Usidharau na wala usifanye kwa kuiga, kwa sababu mtu mwingine alipopata simulizi ile ya jamaa miaka kadhaa mbele, naye akajenga desturi ya kuuacha mlango wake wazi, kitu kilichomponza kwani siku moja wezi walifika na kuiba kila kilichokuwemo.

Unachotakiwa kufanya ni kutokudharau kila unapoliona gazeti mojawapo kati ya Championi, Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda. Hata kama hujanunua wewe, lakini umeliona kipande chake kimetupwa, kiokote, kwani kinaweza kuwa na ile kuponi ya kujishindia nyumba, itakayochezwa mwishoni mwa mwezi huu.

Ukiipata kuponi hiyo, itume kupitia mawakala wa Global Publishers au ipeleke mwenyewe katika ofisi zao zilizopo Bamaga Mwenge kwa wale wa Dar es Salaam.

Nakusisitiza, gazeti la leo ndilo lenye kuponi ya ushindi, ingawa ile ya jana na juzi nazo zinaweza kutenda maajabu. Utaichukua nyumba hii ya kisasa yenye hati, iliyojengwa eneo tulivu na la thamani, kwa shilingi mia tano tu.

Leave a Comment