Christopher Wallace ‘Notorious B.I.G’.
SANAMU ya aliyekuwa rapa marufu, Christopher Wallace ‘Notorious B.I.G’ ambaye kwa sasa ni marehemu inaendelea kutengenezwa ndani ya Jumba la Makumbusho ya Hip Hop Hall of Fame lililopo Brooklyn, New York, Marekani.
Sanamu hiyo inayoonesha sura ya B.I.G kwa ukubwa, inatengenezwa na rapa maarufu huko Brooklyn, Tanda Francis na inasemekeana ikishamalizika itawekwa kwenye eneo la Putnam Triangle Plaza katika mji wa Clinton Hill karibu na mitaa aliyokulia B.I.G ya Bedford-Stuyvesant.
B.I.G alipigwa risasi na kufariki dunia mjini Los Angeles mwaka 1997 akiwa kiongozi wa Kundi la Muziki la East Coast Rap Music.
