Mwanamuziki Chris Brown juzikati alitupia picha yenye tatuu ya picha ya mwanaye Royalty ambayo ameichora mgongoni mwake kisha akashea kwa mashabiki zake maumivu ya kuwa baba.
Jamaa huyo huwa anapenda kuelezea jinsi anavyouvaa ubaba na kuwataka watu wengine wajue kuwa, amebadilika na kuwa mwanaume wa pekee.
Chris Brown na mwanaye Royalty
Bila kujali maumivu anayoyapata katika uchoraji wa tatuu, Chris alitupia picha akiwa kwenye kiti cha mchoraji ambaye alikuwa akimchora kwa wakati huo.
Hata hivyo, baada ya kuwahabarisha watu kinachoendelea alitoa mara moja picha hizo alizozitupia kwenye ukurasa wake wa Instagram.
