
RAPA maarufu kutoka pande za Marekani, Belcalis Marlenis Almánzar ‘Cardi B’ amesema kuwa ana mpango wa kufuata nyayo za msanii mwenzake Amber Rose kwa kuchora tattoo ya jina la mtoto wake wa kiume kwenye uso wake.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Cardi amesema; “Random but…. I’m 1% close too tatting my sons name on my face…. I really really wanna do it!”.
Ikumbukwe kuwa, mpaka sasa Cardi B na mume wake Offset hawajaweka wazi jina la mtoto wao wa kiume mwenye miezi minne.