Msanii wa sinema za Kibongo na mjasiriamali, Devotha Mbaga amekumbwa na bomoabomoa kufuatia nyumba yake kuwa karibu na barabara.
Akizungumza na mwanahabari wetu, nyumbani kwake Kigamboni, Devotha alisema serikali imeweka alama ya X kwenye nyumba yake pamoja na baa kwa kuwa ipo karibu na barababara ambayo inatakiwa kupanuliwa.
“Ndiyo hivyo hatujui kama watatulipa au vipi tunafuatilia serikalini lakini wameshatupigia X. Inaniuma maana kama baa yangu ndiyo kwanza nilikuwa nimekamilisha kujenga ghorofa,” alisema Devotha.
