×

Nay akunwa na uwezo wa Sanjay Boy!

nayMWANDISHI WETU

STAA wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki amefunguka kuwa ameguswa na uwezo wa bwa’m-dogo anayefanya poa kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Andrew John ‘Sanjay Boy’ na kumtabiria mema.

Akizungumzia kipaji cha bwa’mdogo huyo ambaye tayari ana nyimbo nne katika studio mbalimbali ikiwemo C9 Records, MK Records na Mazuu Records, amesema anaamini kama atapewa nafasi, akawezeshwa, atafika mbali.

“Ni suala la muda na kuwezeshwa, dogo anajua nimemsikiliza. Watanzania wampe sapoti, nina imani atatoboa,” alisema Nay.

Dogo huyo anatamba na Wimbo wa Baby aliofanya na Mmarekani M Kingston.

Leave a Comment