
BAADA ya kumshuhudia mwanamama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni raia wa nchini Uganda akitangazwa kuwa Balozi wa Utalii nchini, komediani wa Kenya, Eric Omondi naye amelamba ubalozi Bongo.
Manisapaa ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam kupitia kwa meya wake, Abdallah Mtinika imempa Eric Omondi.
jukumu la kuitangaza manispaa hiyo ambayo ina mambo mengi ukiwemo utalii.
Swali linaloulizwa na wengi ni kwa nini mastaa wa Bongo wanaachia fursa hizi zinakwenda kwa wageni wakati wana uwezo mkubwa wa kuzitumikia?
STORI NA SIFAEL PAUL | GPL
View this post on Instagram