×

Tanzania Kushiriki Miaka 65 Ya Jundokan Karate 2018, Japan

Magwiji wa karate duniani wakiwa katika kongamano la Karate  European Jundokan  Gasshuku 2016 Magwiji wa karate duniani wakiwa katika kongamano la Karate  European Jundokan  Gasshuku 2016.

Sensei Rumadha Fundi aliwakilisha bara la Afrika katika kongamano la wataalamu Karate !

TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN  KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza la OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION” lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu magwiji wa karate lilifanyika Lisabon,Ureno.

Miyazaki Sensei 5 Dan aliyekulia katika Jundokan dojo tokea yupo shule us vududu  Kindergarten huko Okinawa Sensei Rumadha kati na Sensei KinjoMiyazaki Sensei 5 Dan aliyekulia katika Jundokan dojo tokea yupo shule us vududu  Kindergarten huko Okinawa Sensei Rumadha kati na Sensei Kinjo

Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.

Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.

Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate ” European Jundokan  Gasshuku 2016″.

Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha Fundi mtanzania anayetambuliwa na baraza la mchezo la dunia lenye makao kule Okinawa JapanMwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha Fundi mtanzania anayetambuliwa na baraza la mchezo la dunia lenye makao kule Okinawa Japan

Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho ” OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION” imefanya mabadiliko hivi karibuni yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa katika michezo ya  Olympics.
Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayo onekana katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.

Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi,  zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani Okinawa duniania kote.
Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayo tambulika na ” BUDOKAN” kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu ( Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa,Japan.

Tunatumaini kwamba chama cha “JUNDOKAN SO HONBU” kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Afrika mashariki na Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza. Alimalizia hivyo; sensei Rumadha

Leave a Comment