×

Wa kumnusuru Ray C ni Mungu Tu!

Ray-C Rehema Chalamila ‘Ray C’

MUSA MATEJA

TUMUOMBEENI Ray C kwa sababu wa kunusuru maisha yake kwa sasa ni Mungu tu! Ndivyo walivyosikika wakisema baadhi ya mashabiki wa staa wa kike wa Bongo Fleva aliyetamba vilivyo enzi zake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya kumuona akiwa ‘amechizika’, akitaka kuvua nguo hadharani na kujichoma kisu ili afe kabla ya kuokolewa na polisi.

RAYC.jpgKwa kumbukumbu, ilikuwa wikiendi iliyopita Mtaa wa Togo, Kinondoni-Manyanya, Dar karibu na American Chipsi ambapo Ray C alifika akiwa na rafiki yake na kuanza kuzungumza mambo yasiyoeleweka huku akipiga kelele kuwa kuna watu wanataka kumteka.

Hata hivyo, baada ya kuona hali hiyo huku akijigar-agaza kwenye matope, polisi walifika na kumkamata kisha kumpeleka Hospitali ya Mwanan-yamala kwa matibabu kwani wengi walidhani alikuwa kichaa.

ray cRay C alivyosaidiwa na polisi hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari wa Mwananyamala (jina tunalo), Ray C hakuwa amepata kichaa bali alikuwa amelewa kupita kiasi.

Baada ya kuona hivyo, hatimaye mwanadada huyo alipelekwa Sober House iliyopo Bagamoyo, Pwani ambako alikuwa akitibiwa msanii mwenzake, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ ikielezwa kuwa hali yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ akichanganya na pombe ndivyo vinavyotaka kumtoa uhai.

“Madaktari walijaribu kwa kadiri ya uwezo wao kumnusuru Ray C lakini hakutaka kuwasikia hivyo wakam-wachia Mungu. Ndiyo waliomba apelekwe Sober House kwani akiendelea kukaa mitaani hawezi kupona,” alisema daktari huyo.

Tukio la Ray C kupelekwa Sober House lilifanyika usiku wa Juni 16, mwaka huu ambako alipokelewa salama akiambatana na mama yake mzazi na watu wengine.

Ilielezwa kuwa kuwa staa huyo naye  amelazimika kupelekwa huko kutokana na kutibiwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani sehemu alizokuwa akitibiwa zimeonekana zilikuwa zinampa uhuru kiasi kwamba kupona ilikuwa ni ngumu kwake kwani alirudia uvutaji wa madawa hayo.

“Kiukweli Ray C ameshindikana kutibiwa Mwananyamala na badala yake imelazimika apelekwe Bagamoyo kwenye rehab aliyokuwa akitibiwa Chid Benz,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kupewa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Ruge Mutahaba ambaye ni mmoja wa waliowahi kuwa wasimamizi wa Ray C kwa lengo la kutaka kuthibitisha kama kweli Ray C amepelekwa Bagamoyo.

Katika mazungumzo yake na gazeti hili, Ruge alikiri kuwa walilazimika kufanya hivyo baada ya Ray C kuridhia hivyo na zoezi hilo lilifanyika chini ya mama yake mzazi ambaye pia alikuwepo hospitalini hapo.

“Ni kweli baada ya kuambiwa Ray C kakamatwa akiwa amedata, kweli nilishtuka sana na kuuliza alipo hivyo baada ya kuambiwa yupo Mwananyamala nilikwenda pale nikakutana na madaktari, wakaniambia kuwa Ray C hajadata zaidi alikunywa pombe kupita kiasi.

“Niliongea naye (Ray C) mwenyewe akaridhia tumpeleke Bagamoyo kule Soba House ambapo Kalapina na mama yake mzazi (mama Ray C) waliambatana naye kumpeleka huko,” alifunguka Ruge na kuahidi kufuatilia maendeleo ya afya ya mwanadada huyo.

Mapema mwaka huu ni gazeti hili lililoripoti juu ya Ray C kurudia unga lakini yeye na ‘wanaomd-anganya’ kuwa wanampenda walikuja juu wakidai kwamba habari hizo zilikuwa za uongo.

Leave a Comment