×

Trump Nusura Auawe Las Vegas

357144C600000578-3651241-image-a-2_1466459382293 Michael Sandford baada ya kudakwa na polisi.

Las Vegas, Marekani

MGOMBEA urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republica, Donald Trump amenusurika kufa hivi karibuni baada ya mwanamume mmoja raia wa Uingereza aliyetambuliwa kwa jina la Michael Sandford kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Trump na kujaribu kumuua mwanasiasa huyo.

160621023410_michael_steven_sandford__512x288__nocreditMichael Sandford amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican na kusema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na nia ya kumpiga risasi Bw Trump siku ya Jumamosi.

Donald-TrumpDonald Trump

Awali Donald Trump alimtimua Maneja wake wa kampeni Corey Lewandowski kwa kutofautana naye katika kauli zake.

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemlaum Trump kwamba kauli zake ni za hatari na zinaweza kumsababishia madhara baadaye.

Leave a Comment