×

Tyga: Kiki za Mapenzi Zilinifelisha!

kylie-jenner-tyga-split-up

NEW YORK, Marekani

STAA wa Muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Micheal Ray Stevenson ‘Tyga’ kwa mara ya kwanza tangu atemane na mpenzi wake, Kylie amefunguka kuwa kiki za mapenzi zilimfanya kupotea kwenye gemu ya muziki.

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ, Tyga ambaye yupo katika kutambulisha wimbo wake mpya wa 1of1 alisema;

“Uhusiano wangu kwanza ulikuwa wa wazi sana na sehemu kubwa ya kazi zangu za muziki na dili zingine nilizokuwa nikifanya zilipendwa kwa sababu watu waliona mambo yangu ya mapenzi tu na siyo kazi zangu.”

Tyga pia anasema yeye na Kylie bado marafiki na walikuwa pamoja kwenye kufanya video yake mpya ya 1of1 huko Kingston, Jamaica.

 

CREDIT: Andrew Carlos/GPL

Leave a Comment