×

Ini Edo anasa mimba

ini edo.jMKONGWE kunako filamu Nigeria, Iniobong Edo ‘Ini Edo’ amenasa mimba kutoka kwa mchumba wake mpya ambaye ni staa wa filamu Nollywood, Mike Godson.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na staa huyo ambaye aliwahi kubamba na filamu za kuhuzunisha kama Breath Again na Living in Tears, kwa sasa staa huyo hajaziona siku zake (hedhi) kwa takriban miezi mitatu.

“Muda wowote kuanzia sasa ataondoka Nigeria na kukimbilia kwenda kuishi Marekani ama Uingereza

hadi atakapojifungua,” kiliweka nukta chanzo hicho.

Ini aliolewa Novemba 2008 na mfanyabiashara, Philip Ehiagwina lakini walikuja kuachana baada ya miaka mitano ambapo Philip aliamua kuoa mwanamke mwingine, Ruth ambapo Ini aliamua kuwa singo kabla ya kumpata, Mike mwaka jana.

 

Leave a Comment