Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala (Katikati) akifafanua jambo kuhusu maswala ya mateso na dhuluma yanayoendelea kurepotiwa kutoka nchi ya palestina ambapo amewataka watanzania na dunia kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanawatetea wananchi wa Palestina wanaonyanganywa haki yao ya kukaa kwa amani katika nchi yao.
Sheikh Jalala akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea uazimisha siku ya QUDS duniani ambayo ni siku maalum ya kukumbuka mateso wanayokumbana nayo wananchi wa palestina amesema kuwa imefikia wakati sasa dunia kwa pamoja kuungana bila kujali Dini na itikadi zake na kupigania haki ya wapalestina kwani wanaoteseka kule sio waislam pekee bali ni wananchi wote na hata wale wasio na dini.
Profesa Abdul Sharifu ni mstafu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo katika mkutano huo na wahabari naye alipata nafasi ya kueleza chanzo cha mgogoro kati ya mataifa hayo mawili na jinsi gani kwa sasa unaathiri maisha ya wana palestina kwa ujumla.
Nice Munisi ni mmoja kati ya watanzania wachache waliowahi kunafya ziara katikia nchi ya palestina na kujionea ukubwa wa mgogoro huo ambapo hapa akisimumua ushughuda wake kuhusu yale aliyojionea nchini palestina ambapo amesema kuwa alichokiona ni mateso makubwa sana wanayokumbana nayo wananchi wa palestina na dhuluma kubwa kutoka kwa Taifa la Israel hivyo akaendelea kuunga mkono Juhudi za kuunganisha dunia ili kuwatetea wananchi hao amabo hawana hatia lakini wanakumbana na mateso makubwa.
WAPALESTINA waishio nchini wataungana na Wapalestina wenzao na watu mbalimbali kote Duniani kuhadhimisha siku ya Quids Ijumaa Julai mosi ambapo watakuwa na matembezi yatakayoanzia Ilala Boma hadi viwanja vya Tipo Kigogo.
Quids ni siku ya Wapalestina na ukombozi wa mwanadamu Duniani kutoka katika uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji wa mwanadamu.
Kiongozi Mkuu wa Waislam, Dhahebu la Shia Ithnasheriya Tanzania, Sheikh, Hemed Jalala amesema, mahadhimisho hayo yanalenga kuhamasisha amani katika nchi hiyo na kuwasaidia wapalestina wapate ukombozi.
“Palestina imekuwa katika dhuluma, unyanyasaji na ukandamizwaji kwa zaidi ya miaka 60 sasa ambao umekuwa ukifanywa kwa Waislamu na wasio Waislamu.
“Nina imani kama amani, maelewano, upendo na mshikamano utapatiakana Palestina basi utaenea na kusambaa duniani kote, ninawaomba viongozi, waumini na wapigania haki na amani kupigania amani katika aridhi ya Palestina ambayo imekuwa ikidhulumiwa hadi kwao.
“Mahadhimisho hayo yatafanyika Julai 1 ambapo kutakuwa na matembezi ya amani kutoka ,”alisema Jalala.