×

Afya ya Kiongozi wa Korea Kaskazini ipo matatani

kim_jong-un_watch_test_640x360_reuters_nocreditNa Leonard Msigwa

Afya ya kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini, Kim Jong ipo matatani baada ya kuripotiwa kusumbuliwa na maradhi ya insomnia. Kim Jong aliyechukua madaraka toka kwa baba yake aliyefariki mwaka 2011. Anafahamika kwa ubabe wake wa kuongoza nchi hiyo kimabavu na kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

“Kim Jong ameongezeka uzito wa mwili kwa zaidi ya kilo 40 toka aanze kuliongoza taifa hilo tukutu miaka minne iliyopita, hali hiyo imetokana na kula sana pamoja na kunywa pombe kupita kiasi” alisema jasusi wa kujitegemea toka Korea Kusini wiki iliyopita.North Korean leader Kim Jong Un gives field guidance to the newly built Wisong Scientists Residential District in this undated photo released by North Korea's Korean Central News Agency (KCNA) in Pyongyang October 14, 2014. Kim, shown using a cane for support, re-appeared in state media on Tuesday after a lengthy public absence that had fuelled speculation over his health and grip on power in the secretive, nuclear-capable country. REUTERS/KCNA (NORTH KOREA - Tags: POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY) ATTENTION EDITORS - THIS PICTURE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. REUTERS IS UNABLE TO INDEPENDENTLY VERIFY THE AUTHENTICITY, CONTENT, LOCATION OR DATE OF THIS IMAGE. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. NO THIRD PARTY SALES. NOT FOR USE BY REUTERS THIRD PARTY DISTRIBUTORS. SOUTH KOREA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SOUTH KOREA - RTR4A38M

Pia kiongozi huyo kijana anasumbuliwa na maradhi ya insomnia na serikali ya mjini Seoul imekuwa ikifanya siri kuhusu maradhi hayo. Shirika la Kijasusi la Taifa la The National Intelligence Service (NIS) lilitoa taarifa hiyo ya maradhi kwa siri kwenye Kamati ya Bunge la nchi hiyo.

Alipochukua madaraka toka kwa marehemu baba yake mwaka 2011 inakadiriwa alikuwa na uzito wa kilo 90 hadi kufika mwaka 2014 alikuwa na kilo 120 na mwaka huu imedhibitishwa amefikisha kilo 130 ambazo si rafiki sana kwa afya ya binadamu.

Mwanasheria wa chama tawala cha nchi hiyo Lee Cheol-Woo aliwaambia waandishi wa habari baada ya kupokea taarifa ya NIS, “maelezo ya NIS wanasema anaumwa insomnia.”

31 Jan 2015 --- (150131) -- PYONGYANG, Jan. 31 (Xinhua) -- Photo provided by Korean Central News Agency (KCNA) on Jan. 31, 2015 shows top leader of the Democratic People's Republic of Korea (DPRK) Kim Jong Un (front) inspecting a drill of the Korean People's Army (KPA). The fighter airmen and combined submarine units successively carried out the drill. Kim Jong Un gave instructions for bolstering up the operation capabilities of the units of all services. He said that the DPRK is ready to counter any war includ --- Image by © KCNA/Xinhua Press/CorbisLee aliongeza “kwasasa yupo makini kuimarisha usalama wa afya yake na taifa kwa ujumla kwa kutumia jeshi ambalo ana imani nalo kuongoza nchi yao endapo hali yake itazidi kudhohofika.”

“Kutokana na kupenda kwake kula sana pamoja na kunywa pombe kupitiliza, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele anazidi kudhohofu,” alisema Lee.

Mbali na kuwa mnene kuptiliza ni kawaida kuonekana na kipande cha sigara mkononi anapokagua mashamba, shughuli za ujenzi na mimea.

Baba yake marehemu Kim Jong-II na babu yake Kim II-Sung wote walikuwa na maradhi ya unene uliopitiliza na wavutaji wakubwa wa sigara hali iliyopelekea wote wafariki kwa ugonjwa wa shinikizo la moyo.

Pia shirika la kijasusi la nchini humo NIS limedhibitisha shangazi yake mwenye ushawishi mkubwa nchi Korea Kaskazini  Kim Kyong-Hui bado mzima. Japo amepotea kwa muda mrefu sana mbele ya jamii baada ya kifo cha mumewe Jang Song-Taek, aliyenyongwa baada ya kutuhumiwa na Kim Jong kutaka kuipindua serikali yake na makosa ya rushwa.

” amekuwa mlevi sugu toka kifo cha mumewe aliyenyongwa mwaka 2013, lakini kwa sasa anaendelea vyema chini ya uangalizi maalum kwenye makazi yake mjini Pyongyang” alisema Lee.

Shangazi yake Kim Jong na mumewe walionekana kama viongozi wenye nguvu nchini Korea Kaskazini watakaomsaidia na kumshauri Kim Jong kuiongoza nchi hiyo kutokana na kurithi uongozi wa marehemu baba yake akiwa bado na umri mdogo. Matarajio ambayo yaliyeyuka baada ya Jang Song-Taek kukutwa na hatia ya rushwa na njama za kumpindua Kim Jong. Kuendelea kuugua kwa shangazi yake ni pigo kubwa sana kwa Kim Jong ambaye bado anahitaji kusimamiwa kuliongoza taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kijeshi.

Leave a Comment