×

Sigara na Mshumaa vyasababisha vibanda 500 kuteketea

msangiKamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

Sengerema, Mwanza

KATIKA matukio mawili tofauti moto umeteketeza vibanda zaidi ya  500 vya biashara visiwani Kabiga na Migongo wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

moto.jpg

Akizungumza kuhusu matukio hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa katika Kisiwa cha Kabiga Kata ya Maisome zaidi ya vibanda 300 viliteketea Alhamisi wakati wafanyabiashara walipokuwa wakigawana mafuta ya petroli yanayodaiwa kuibwa.

Amesema mmoja wa wafanyabiashara hao aliagusha kipande cha sigara kilichowashwa ndipo moto ulipolipuka. Amesema katika Kisiwa cha Migongo Kata ya Maisome, zaidi ya vibanda 200 viliteketea jana usiku chanzo kikiwa ni mshumaa.

Leave a Comment