Dar es Salaam
Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo (TIB) Profesa William Lyakurwa.
Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma, Rais amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria ametengua uteuzi wa Wajumbe TIB.
Dk Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu, Brigedia Mabula Mashauri, Dk Razack Lokina, Rose Aiko, Profea Joseph Bwechweshaija, Said Seif Mzee, Dk Arnold Kihaule, Maduka Kessy na Charles Singili. Uteuzi unaanza leo.

