MKALI wa Ngoma ya Chafu Pozi, Bill Nas amefunguka kuwa, ameshangazwa na maneno ya kimahaba yaliyoandikwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Ala Za Roho, kinachoruka kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kuongeza kuwa, hana uhusiano naye.
Akichonga na Ebwana Dah, mwanamuziki huyo alisema kuwa, mtangazaji huyo atakuwa ana lake jambo na si vinginevyo maana yeye hajawahi kumuambia lolote lakini anashangaa kile kinachoendelea kwenye mitandao.
“Siko kwenye uhusiano na Diva, so mimi mwenyewe nimeona kwenye mtandao kaandika maneno kibao ya mahaba lakini hakuna ukweli wowote ule kati yake na mimi,” alisema Bill Nas.
Diva kwenye ukurasa wake wa ‘Insta’ aliandika kuwa, anampenda sana Bill Nas na anajua watu watachonga sana lakini yeye wala hajali.
BILL NASS AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA GODZILLAH
