
Victor Barrio, 29 enzi za uhai wake.
Hivi ndvyo Victor Barrio alivyopigwa na ng’ombe.
Mchezaji maarufu wa kucheza na ng’ombe “Bullfighter” ameuawa na ng’ombe aliyekuwa akicheza naye kwenye tamasha la michezo ya kucheza na ng’ombe katika Mji wa Terurel huko Aragon nchini Hispania.
Hii ni mara ya kwanza ndani ya karne ya 21 kwa mchezaji kuuliwa nchini humo.
Baada ya tukio hilo, Victor alikimbizwa Hospitali na muda mfupi baadaye alifariki dunia. Kifo chake kimetokana na kugongwa na pembe za ng’ombe sehemu ya kifua.

Mke wa Victor Barrio.
Wakati tukio hilo likitokea mke wa Victor Barrio alikuwa mmoja wa watazamaji aliyehudhuria tamasha hilo mjini Terurel.

