×

Pipi: Ndoa haikusimamisha muziki wangu

pipiMAYASA MARIWATA

M SANII wa Bongo Fleva, Doreen Aurelian Ponera ‘Pipi’ amefungukia ukimya wake wa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote kuwa hakufulia na pia ndoa haikusimamisha muziki wake kama watu wanavyoongelea.

Akichonga na Over Ze Weekend, Pipi ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya ya Hafai akimshirikisha mkali wa Hip Hop Bongo, Nikki wa Pili alisema kuwa shughuli za ujasiriamali anazozifanya ndizo zilizomfanya akayumba.

“Naamini nimerudi upya kama nilivyokuwa zamani kwani ngoma yangu hii ya Hafai nikiwa na Nikki ni majibu ya kila kitu,” alisema Pipi aliyewahi pia kutamba na Wimbo wa Njia Panda akiwa na Barnaba.

Leave a Comment