×

Tunda: Naanzaje kuachanana Young D?

tunda-21.jpg Stori: Imelda Mtema, Wikienda

DAR ES SALAAM: Vunja ukimya! Muuza nyago (video queen) ambaye hivi karibuni alijipatia umaarufu kutokana na vituko vyake kwenye mitandao ya kijamii, Tunda Sabasita amefungukia uzushi unaonea kuwa ameachana na mpenzi wake, David Genzi ‘Young D’.

TUNDA43Tunda aliliambia Wikienda kuwa, hawezi kuachana na mpenzi wake huyo ambaye hivi karibuni alijitangaza hadharani kuwa alijiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

“Jamani naanzaje sasa kuachana na David (Young D)? Nasikia tu watu wanasema nimeachana na David, wajue siyo kitu rahisi kwa sababu ni mtu ambaye nampenda sana,” alisema Tunda.

Leave a Comment