×

Kikosi bora cha Euro 2016 hiki hapa

Ronaldo_missed_a_glorious_chance_to_win_it_for_Portugal_when_he_-a-86_1467322858617Cristiano Ronaldo

MSHAMBULIAJI wa Ureno Cristiano Ronaldo, anayechezea Real Madrid ya Hispania, ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Euro 2016 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa.

rui-patricioRui Patrício

Ronaldo aliwahi kujumuishwa katika kikosi sawa mwaka 2004 na mwaka 2012. Raia mwenzake wa Ureno, Pepe pia yupo kwenye kikosi hicho na aliwahi pia kujumuishwa 2008 na 2012.

joshua_kimmichJoshua Kimmich

Awali, kulikuwa kukitajwa kikosi cha wachezaji 23 lakini wakati huu kumetajwa kikosi cha wachezaji 11.

Jérôme BoatengJérôme Boateng

Kikosi kamili kinajumuisha (4-2-3-1): Rui Patrício (Ureno); Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe (Ureno), Raphaël Guerreiro (Ureno); Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (Ufaransa), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (Ufaransa); Cristiano Ronaldo (Ureno).

Antoine-Griezmann-1Antoine Griezmann

Kikosi hicho kiliteuliwa na jopo la kiufundi cha Uefa lililojumuisha, miongoni mwa wengine, Sir Alex Ferguson na David Moyes.

“Tunaamini kikosi hiki cha wachezaji XI kinawakilisha wachezaji bora zaidi walioshiriki michuano,” amesema, Ferguson, ambaye ni balozi mwema wa ukufunzi wa Uefa.

Leave a Comment