×

Taylor Swift Mwanamuziki Anayelipwa Zaidi Duniani

maxresdefault

 Taylor Swift .

AKIWA na umri wa miaka 26 tu mwanamuziki Taylor Swift wa Marekani ndiye mwanamuziki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kulingana na ripoti ya jarida maarufu la Forbes. Ripoti hiyo iliwekwa hadharani Jumatatu wiki hii ambapo inasema anaingiza kibindoni Dola za Marekani milioni 170.

Kiasi hicho kimepatikana toka Juni 2015 hadi Juni 2016, ikiwa ni mara mbili ya kiasi alichokipata mwaka uliopita. Swift kawazidi wanamuziki wengi maarufu wakiwemo Adele, Bruce Springsteen, Katy Perry, Rihanna na Madonna.

Rihanna-Hot1

 Rihanna.

Kupitia jarida la Forbes, mhariri wake Zack O’Malley amesema sehemu kubwa ya mapato hayo yametokana na maonyesho ya jukwaani. Taylor Swift alifanya ziara ndefu aliyoipa jina la “1989 World Tour” na kuzunguka miji mikubwa duniani iliyomwingizia kipato kikubwa.

👀

A photo posted by Taylor Swift (@taylorswift) on

 

Leave a Comment