×

Sumaye Kugombea Uenyekiti Chadema

Sumaye

Frederick Sumaye.

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amekubali ombi la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani, waliomchukulia fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kanda hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Baadhi ya viongozi hao waliojitokeza kumchukulia fomu Sumaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa chama hicho Ilala, Dk. Makongoro Mahanga na Mwenyekiti wa mkoa wa Pwani, Baraka Mwago.

Sumaye+Photo

Baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za Chadema Kanda ya Kinondoni jana, viongozi hao walielekea nyumbani kwa Sumaye maeneo ya Tondoroni Kiluvya, mkoa wa Pwani, kwa ajili ya kumkabidhi.

Baada ya kupokea fomu hizo, Sumaye alikubali ombi hilo na kuzijaza na kuahidi kurejesha leo katika ofisi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Waitara, Sumaye alisema ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi vitongojini.

From left, Former Prime Minister Fredrick Sumaye speaks during a press conference in Mwanza yesterday, about a move by Police banned from paying their last respects to Chadema Geita region chairman the late Alphonce Mawazo. Zanzibar Party’s Vice Chairman, Said Issa Mohamed, National Chairman, Freeman Mbowe, and October general election Party’s candidate, Edward Lowassa. PHOTO|MICHAEL JAMSON

Waziri Mkuu huyo mstaafu alihamia upinzani mwaka jana katika harakati za uchaguzi mkuu akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivi karibuni aliteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Sasa atagombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Leave a Comment