×

Mastaa wanaovuma kwa nyota za wenzao

KanumbaSteven Kanumba enzi za uhai wake.

STORI: GABRIEL NG’OSHA

Ni kweli kila mwanadamu ana nyota yake lakini baadhi ya mastaa Bongo wanatembelea nyota za wenzao kwani hawakuwa maarufu kwa majina yao bali kwa majina ya wengine. Wapo wengi lakini leo kwa ufupi nikutajie wafuatao;

Nuh (2)Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ kushoto akiwa na Nuh mziwanda.

JIKE SHUPA; NYOTA YA SHILOLE

Kuibuka kwa mwanadada Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ kwenye video ya wimbo wa zilipendwa wa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Nuh Mziwanda kulizua utata sana juu ya dada huyo kudaiwa kuigiza tabia za Shilole alizokuwa akizifanya kwa Mziwanda kwani Jike Shupa anafanana na Shilole kama pacha wake na majina yao yanashabihiana, mmoja Zena mwingine Zuwena.

Rammy GalisRammy Galis

RAMMY GALIS; NYOTA YA KANUMBA

Mwigizaji Rammy Galis alianza kung’ara mara baada ya msanii nguli wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba kufariki dunia. Kuliibuka wasanii wengi wakidai kufanana kwa muonekano pamoja na uingizaji kama ilivyokuwa Kanumba.

WESTWOOD, CA - APRIL 21: Nicki Minaj arrives at the "The Other Woman" - Los Angeles Premiere at Regency Village Theatre on April 21, 2014 in Westwood, California. (Photo by Steve Granitz/WireImage)Nick Minaj

Miongoni mwao ni Rammy ‘Pacha wa Kanumba’ ambaye anadai kufanana vilivyo na Kanumba na hata viatu vyake vinamtosha.

tammy (1)Tammy Ally ‘Nick Minaji wa Bongo

TAMMY; NYOTA YA NICK MINAJ

Kutokana na kujaaliwa shepu f’lani hivi, Mwanamuziki Tammy Ally ‘Nick Minaji wa Bongo, amejibatiza jina hilo kwa sababu tu ya shepu yake kufanana na mwanamuziki wa Kimarekani, Nick Minaj.

amber lulu Lulu Auggen ‘Amber Lulu’

AMBER LULU; NYOTA YA AMBER ROSE

Mdada wa mjini Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ anaendelea kung’ara mjini kwa swaga zake kama za mwanamitindo machachari wa Marekani Amber Rose.

amberAmber Rose.

Muonekano wa Amber Lulu ni kama ule wa Amber Rose kwani kuanzia nywele, shepu, mitindo ya utupuu-tupu kwenye mapozi ya picha ni ule ule.

Leave a Comment